Isaya 26:3
Isaiah 26:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
Isaiah 26:3 in English
Isaiah 26:3 · Berean Standard Bible
You will keep in perfect peace the steadfast of mind, because he trusts in You.
Context
1Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda:
Tuna mji ulio na nguvu,
Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake. 2Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia,
taifa lile lidumishalo imani. 3Utamlinda katika amani kamilifu
yeye ambaye moyo wake ni thabiti
kwa sababu anakutumaini wewe. 4Mtumaini Bwana milele,
kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele. 5Huwashusha wale wajikwezao,
huushusha chini mji wenye kiburi,
huushusha hadi ardhini
na kuutupa chini mavumbini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.