Isaya 14:26
Isaiah 14:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote, huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.
Isaiah 14:26 in English
Isaiah 14:26 · Berean Standard Bible
This is the plan devised for the whole earth, and this is the hand stretched out over all the nations.
Context
24Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa,
“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,
nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. 25Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,
juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.
Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,
nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” 26Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,
huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote. 27Kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amekusudia,
ni nani awezaye kumzuia?
Mkono wake umenyooshwa,
ni nani awezaye kuurudisha? 28Neno hili lilikuja mwaka ule Mfalme Ahazi alipofariki:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.