Isaya 14:24
Isaiah 14:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa, “Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa, nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama.
Isaiah 14:24 in English
Isaiah 14:24 · Berean Standard Bible
The LORD of Hosts has sworn: “Surely, as I have planned, so will it be; as I have purposed, so will it stand.
Context
22Bwana Mwenye Nguvu Zote asema,
“Nitainuka dhidi yao,
nitalikatilia mbali jina lake kutoka Babeli pamoja na watu wake walionusurika,
watoto wake na wazao wake,”
asema Bwana. 23“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi,
na kuwa nchi ya matope;
nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 24Bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa,
“Hakika, kama vile nilivyopanga, ndivyo itakavyokuwa,
nami kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyosimama. 25Nitamponda Mwashuru katika nchi yangu,
juu ya milima yangu nitawakanyagia chini.
Nira yake itaondolewa kutoka kwa watu wangu,
nao mzigo wake utaondolewa kutoka mabegani mwao.” 26Huu ndio mpango uliokusudiwa kwa ajili ya ulimwengu wote,
huu ni mkono ulionyooshwa juu ya mataifa yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.