Isaya 13:6
Isaiah 13:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ombolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu, itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.*
Isaiah 13:6 in English
Isaiah 13:6 · Berean Standard Bible
Wail, for the Day of the LORD is near; it will come as destruction from the Almighty.*
Context
4Sikilizeni kelele juu ya milima,
kama ile ya umati mkubwa wa watu!
Sikilizeni, makelele katikati ya falme,
kama mataifa yanayokusanyika pamoja!
Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya
jeshi kwa ajili ya vita. 5Wanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
Bwana na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote. 6Ombolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.* 7Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka. 8Hofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwaka kama moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.