Isaya 13:7
Isaiah 13:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea, moyo wa kila mtu utayeyuka.
Isaiah 13:7 in English
Isaiah 13:7 · Berean Standard Bible
Therefore all hands will fall limp, and every man’s heart will melt.
Context
5Wanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
Bwana na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote. 6Ombolezeni, kwa maana siku ya Bwana i karibu,
itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.* 7Kwa sababu ya hili, mikono yote italegea,
moyo wa kila mtu utayeyuka. 8Hofu itawakamata,
uchungu na maumivu makali yatawashika,
watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa.
Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake,
nyuso zao zikiwaka kama moto. 9Tazameni, siku ya Bwana inakuja,
siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali,
kuifanya nchi kuwa ukiwa
na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.