Isaya 1:29
Isaiah 1:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni ambayo mlifurahia, mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
Isaiah 1:29 in English
Isaiah 1:29 · Berean Standard Bible
Surely you will be ashamed of the sacred oaks in which you have delighted; you will be embarrassed by the gardens that you have chosen.
Context
27Sayuni itakombolewa kwa haki,
wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu. 28Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa,
nao wanaomwacha Bwana wataangamia. 29“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni
ambayo mlifurahia,
mtafadhaika kwa sababu ya bustani
mlizozichagua. 30Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka,
kama bustani isiyokuwa na maji. 31Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto,
na kazi yake kama cheche ya moto;
vyote vitaungua pamoja,
wala hakuna wa kuuzima huo moto.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.