Hosea 9:8
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nabii, pamoja na Mungu wangu, ndiye mlinzi juu ya Efraimu, hata hivyo mitego inamngojea katika mapito yake yote, na uadui katika nyumba ya Mungu wake.
Hosea 9:8 in English
Hosea 9:8 · Berean Standard Bible
The prophet is Ephraim’s watchman, along with my God,* yet the snare of the fowler lies on all his paths. Hostility is in the house of his God!
Context
6Hata ikiwa wataokoka maangamizi,
Misri atawakusanya,
nayo Memfisi* itawazika.
Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma,
nayo miiba itafunika mahema yao. 7Siku za adhabu zinakuja,
siku za malipo zimewadia.
Israeli na afahamu hili.
Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana
na uadui wenu ni mkubwa sana,
nabii anadhaniwa ni mpumbavu,
mtu aliyeongozwa na Mungu
anaonekana mwendawazimu. 8Nabii, pamoja na Mungu wangu,
ndiye mlinzi juu ya Efraimu,
hata hivyo mitego inamngojea
katika mapito yake yote,
na uadui katika nyumba ya Mungu wake. 9Wamezama sana katika rushwa,
kama katika siku za Gibea.
Mungu atakumbuka uovu wao
na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao. 10“Nilipompata Israeli, ilikuwa kama
kupata zabibu jangwani;
nilipowaona baba zenu, ilikuwa kama kuona
matunda ya kwanza katika mtini.
Lakini walipofika Baal-Peori, walijiweka wakfu
kwa ile sanamu ya aibu,
nao wakawa najisi
kama kitu kile walichokipenda.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.