Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata ikiwa wataokoka maangamizi, Misri atawakusanya, nayo Memfisi* itawazika. Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma, nayo miiba itafunika mahema yao.

Hosea 9:6 in English

Hosea 9:6 · Berean Standard Bible

For even if they flee destruction, Egypt will gather them and Memphis will bury them. Their precious silver will be taken over by thistles, and thorns will overrun their tents.

Context

4Hawatammiminia Bwana sadaka ya divai wala dhabihu zao hazitampendeza. Dhabihu kama hizo zitakuwa kwao kama mkate wa waombolezaji; nao wote wazilao watakuwa najisi. Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe; kisije katika Hekalu la Bwana. 5Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za Bwana? 6Hata ikiwa wataokoka maangamizi, Misri atawakusanya, nayo Memfisi* itawazika. Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma, nayo miiba itafunika mahema yao. 7Siku za adhabu zinakuja, siku za malipo zimewadia. Israeli na afahamu hili. Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana na uadui wenu ni mkubwa sana, nabii anadhaniwa ni mpumbavu, mtu aliyeongozwa na Mungu anaonekana mwendawazimu. 8Nabii, pamoja na Mungu wangu, ndiye mlinzi juu ya Efraimu, hata hivyo mitego inamngojea katika mapito yake yote, na uadui katika nyumba ya Mungu wake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.