Hosea 9:5
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za Bwana?
Hosea 9:5 in English
Hosea 9:5 · Berean Standard Bible
What will you do on the appointed day, on the day of the LORD’s feast?
Context
3Hawataishi katika nchi ya Bwana,
Efraimu atarudi Misri
na atakula chakula
kilicho najisi huko Ashuru. 4Hawatammiminia Bwana sadaka ya divai
wala dhabihu zao hazitampendeza.
Dhabihu kama hizo zitakuwa kwao
kama mkate wa waombolezaji;
nao wote wazilao watakuwa najisi.
Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe;
kisije katika Hekalu la Bwana. 5Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa,
katika siku za sikukuu za Bwana? 6Hata ikiwa wataokoka maangamizi,
Misri atawakusanya,
nayo Memfisi* itawazika.
Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma,
nayo miiba itafunika mahema yao. 7Siku za adhabu zinakuja,
siku za malipo zimewadia.
Israeli na afahamu hili.
Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana
na uadui wenu ni mkubwa sana,
nabii anadhaniwa ni mpumbavu,
mtu aliyeongozwa na Mungu
anaonekana mwendawazimu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.