Hosea 6:8
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Gileadi ni mji wenye watu waovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu.
Hosea 6:8 in English
Hosea 6:8 · Berean Standard Bible
Gilead is a city of evildoers, tracked with footprints of blood.
Context
6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,
kumkubali Mungu zaidi
kuliko sadaka za kuteketezwa. 7Wamevunja Agano kama Adamu:
huko hawakuwa waaminifu kwangu. 8Gileadi ni mji wenye watu waovu,
umetiwa madoa kwa nyayo za damu. 9Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,
ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;
wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,
wakifanya uhalifu wa aibu. 10Nimeona jambo la kutisha
katika nyumba ya Israeli.
Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba
na Israeli amenajisika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.