Hosea 4:11
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
katika ukahaba, divai ya zamani na divai mpya, ambavyo huondoa ufahamu
Hosea 4:11 in English
Hosea 4:11 · Berean Standard Bible
Promiscuity, wine, and new wine take away understanding.
Context
9Hata itakuwa: Kama walivyo watu,
ndivyo walivyo makuhani.
Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao
na kuwalipa kwa matendo yao. 10“Watakula lakini hawatashiba;
watajiingiza katika ukahaba
lakini hawataongezeka,
kwa sababu wamemwacha Bwana
na kujiingiza wenyewe 11katika ukahaba,
divai ya zamani na divai mpya,
ambavyo huondoa ufahamu 12wa watu wangu.
Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti
nao hujibiwa na fimbo ya mti.
Roho ya ukahaba imewapotosha,
hawana uaminifu kwa Mungu wao. 13Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima
na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,
chini ya mialoni, milibua na miela,
ambako kuna vivuli vizuri.
Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba
na wake za wana wenu uzinzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.