Hosea 2:16
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku ile,” asema Bwana, “utaniita mimi ‘Mume wangu’; hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’
Hosea 2:16 in English
Hosea 2:16 · Berean Standard Bible
In that day,” declares the LORD, “you will call Me ‘my Husband,’* and no longer call Me ‘my Master.’*
Context
14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi;
nitamwongoza hadi jangwani
na kuzungumza naye kwa upole. 15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,
nami nitalifanya Bonde la Akori*
mlango wa matumaini.
Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,
kama siku zile alizotoka Misri. 16“Katika siku ile,” asema Bwana,
“utaniita mimi ‘Mume wangu’;
hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’ 17Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake,
wala hataomba tena kwa majina yao. 18Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao
na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,
na viumbe vile vitambaavyo ardhini.
Upinde, upanga na vita,
nitaondolea mbali katika nchi,
ili kwamba wote waweze kukaa salama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.