Hosea 2:14
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa hiyo sasa nitamshawishi; nitamwongoza hadi jangwani na kuzungumza naye kwa upole.
Hosea 2:14 in English
Hosea 2:14 · Berean Standard Bible
“Therefore, behold, I will allure her and lead her to the wilderness, and speak to her tenderly.
Context
12Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake,
ambayo alisema yalikuwa malipo yake
kutoka kwa wapenzi wake;
nitaifanya kuwa kichaka,
nao wanyama pori wataila. 13Nitamwadhibu kwa ajili ya siku
alizowafukizia uvumba Mabaali;
alipojipamba kwa pete
na kwa vito vya thamani,
na kuwaendea wapenzi wake,
lakini mimi alinisahau,”
asema Bwana. 14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi;
nitamwongoza hadi jangwani
na kuzungumza naye kwa upole. 15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,
nami nitalifanya Bonde la Akori*
mlango wa matumaini.
Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,
kama siku zile alizotoka Misri. 16“Katika siku ile,” asema Bwana,
“utaniita mimi ‘Mume wangu’;
hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.