Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu, nami nitalifanya Bonde la Akori* mlango wa matumaini. Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake, kama siku zile alizotoka Misri.

Hosea 2:15 in English

Hosea 2:15 · Berean Standard Bible

There I will give back her vineyards and make the Valley of Achor * into a gateway of hope. There she will respond as she did in the days of her youth, as in the day she came up out of Egypt.

Context

13Nitamwadhibu kwa ajili ya siku alizowafukizia uvumba Mabaali; alipojipamba kwa pete na kwa vito vya thamani, na kuwaendea wapenzi wake, lakini mimi alinisahau,” asema Bwana. 14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi; nitamwongoza hadi jangwani na kuzungumza naye kwa upole. 15Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu, nami nitalifanya Bonde la Akori* mlango wa matumaini. Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake, kama siku zile alizotoka Misri. 16“Katika siku ile,” asema Bwana, “utaniita mimi ‘Mume wangu’; hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’ 17Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake, wala hataomba tena kwa majina yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.