Hosea 13:3
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.
Hosea 13:3 in English
Hosea 13:3 · Berean Standard Bible
Therefore they will be like the morning mist, like the early dew that vanishes, like chaff blown from a threshing floor, like smoke through an open window.
Context
1Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka,
alikuwa ametukuzwa katika Israeli.
Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali
naye akafa. 2Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi;
wanajitengenezea sanamu
kutokana na fedha yao,
vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari,
vyote kazi ya fundi stadi.
Inasemekana kuhusu hawa watu,
“Hutoa dhabihu za binadamu
na kubusu sanamu za ndama.” 3Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi,
kama umande wa alfajiri utowekao,
kama makapi yapeperushwayo
kutoka sakafu ya kupuria nafaka,
kama moshi utorokao kupitia dirishani. 4“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu,
niliyewaleta ninyi toka Misri.
Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,
hakuna Mwokozi isipokuwa mimi. 5Niliwatunza huko jangwani,
katika nchi yenye joto liunguzalo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.