Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

Hosea 13:4 in English

Hosea 13:4 · Berean Standard Bible

Yet I am the LORD your God ever since the land of Egypt; you know no God but Me, for there is no Savior besides Me.

Context

2Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi; wanajitengenezea sanamu kutokana na fedha yao, vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari, vyote kazi ya fundi stadi. Inasemekana kuhusu hawa watu, “Hutoa dhabihu za binadamu na kubusu sanamu za ndama.” 3Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani. 4“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi. 5Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo. 6Nilipowalisha, walishiba, waliposhiba, wakajivuna, kisha wakanisahau mimi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.