Waebrania 6:15
Hebrews 6:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.
Hebrews 6:15 in English
Hebrews 6:15 · Berean Standard Bible
And so Abraham, after waiting patiently, obtained the promise.
Context
13Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 14akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 15Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa. 16Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 17Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.