Native Bible

Hebrews 6:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote.

Hebrews 6:16 in English

Hebrews 6:16 · Berean Standard Bible

Men swear by someone greater than themselves, and their oath serves as a confirmation to end all argument.

Context

14akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 15Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa. 16Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 17Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo. 18Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.