Waebrania 6:13
Hebrews 6:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake,
Hebrews 6:13 in English
Hebrews 6:13 · Berean Standard Bible
When God made His promise to Abraham, since He had no one greater to swear by, He swore by Himself,
Context
11Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 12ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi. 13Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 14akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 15Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.