Waebrania 1:10
Hebrews 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia asema, “Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
Hebrews 1:10 in English
Hebrews 1:10 · Berean Standard Bible
And: “In the beginning, O Lord, You laid the foundations of the earth, and the heavens are the work of Your hands.
Context
8Lakini kwa habari za Mwana asema,
“Kiti chako cha enzi, Ee Mungu,
kitadumu milele na milele,
nayo haki itakuwa fimbo ya utawala
ya ufalme wako. 9Umependa haki na kuchukia uovu;
kwa hiyo Mungu, Mungu wako,
amekuweka juu ya wenzako
kwa kukupaka mafuta ya furaha.” 10Pia asema,
“Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. 11Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu;
zote zitachakaa kama vazi. 12Utazikungʼutakungʼuta kama joho,
nazo zitachakaa kama vazi.
Lakini wewe hubadiliki,
nayo miaka yako haikomi kamwe.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.