Waebrania 1:8
Hebrews 1:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
Hebrews 1:8 in English
Hebrews 1:8 · Berean Standard Bible
But about the Son He says: “Your throne, O God, endures forever and ever, and justice is the scepter of Your kingdom.
Context
6Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema,
“Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.” 7Anenapo kuhusu malaika asema,
“Huwafanya malaika wake kuwa pepo,
watumishi wake kuwa miali ya moto.” 8Lakini kwa habari za Mwana asema,
“Kiti chako cha enzi, Ee Mungu,
kitadumu milele na milele,
nayo haki itakuwa fimbo ya utawala
ya ufalme wako. 9Umependa haki na kuchukia uovu;
kwa hiyo Mungu, Mungu wako,
amekuweka juu ya wenzako
kwa kukupaka mafuta ya furaha.” 10Pia asema,
“Hapo mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.