Habakuki 1:7
Habakkuk 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni watu wanoogopwa na wanaotisha; wenyewe ndio sheria yao, na huinua heshima yao wenyewe.
Habakkuk 1:7 in English
Habakkuk 1:7 · Berean Standard Bible
They are dreaded and feared; from themselves they derive justice and sovereignty.
Context
5“Yatazame mataifa,
uangalie na ushangae kabisa.
Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu
ambacho hungeamini,
hata kama ungeambiwa. 6Nitawainua Wakaldayo,
watu hao wakatili na wenye haraka,
ambao hupita dunia yote
kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe. 7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;
wenyewe ndio sheria yao,
na huinua heshima yao wenyewe. 8Farasi wao ni wepesi kuliko chui,
na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo.
Askari wapanda farasi wao huenda mbio;
waendesha farasi wao wanatoka mbali.
Wanaruka kasi kama tai ili kurarua; 9wote wanakuja tayari kwa fujo.
Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele
kama upepo wa jangwani,
na kukusanya wafungwa
kama mchanga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.