Habakuki 1:5
Habakkuk 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Yatazame mataifa, uangalie na ushangae kabisa. Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu ambacho hungeamini, hata kama ungeambiwa.
Habakkuk 1:5 in English
Habakkuk 1:5 · Berean Standard Bible
“Look at the nations and observe— be utterly astounded!* For I am doing a work in your days that you would never believe even if someone told you.*
Context
3Kwa nini unanifanya nitazame dhuluma?
Kwa nini unavumilia makosa?
Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu;
kuna mabishano na mapambano kwa wingi. 4Kwa hiyo sheria imepotoshwa,
nayo haki haipo kabisa.
Waovu wanawazunguka wenye haki,
kwa hiyo haki imepotoshwa. 5“Yatazame mataifa,
uangalie na ushangae kabisa.
Kwa sababu katika siku zako nitafanya kitu
ambacho hungeamini,
hata kama ungeambiwa. 6Nitawainua Wakaldayo,
watu hao wakatili na wenye haraka,
ambao hupita dunia yote
kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe. 7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;
wenyewe ndio sheria yao,
na huinua heshima yao wenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.