Habakuki 1:9
Habakkuk 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wote wanakuja tayari kwa fujo. Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele kama upepo wa jangwani, na kukusanya wafungwa kama mchanga.
Habakkuk 1:9 in English
Habakkuk 1:9 · Berean Standard Bible
All of them come bent on violence; their hordes advance like the east wind; they gather prisoners like sand.
Context
7Ni watu wanoogopwa na wanaotisha;
wenyewe ndio sheria yao,
na huinua heshima yao wenyewe. 8Farasi wao ni wepesi kuliko chui,
na wakali kuliko mbwa mwitu wakati wa machweo.
Askari wapanda farasi wao huenda mbio;
waendesha farasi wao wanatoka mbali.
Wanaruka kasi kama tai ili kurarua; 9wote wanakuja tayari kwa fujo.
Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele
kama upepo wa jangwani,
na kukusanya wafungwa
kama mchanga. 10Wanawabeza wafalme,
na kuwadhihaki watawala.
Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma;
wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji. 11Kisha wanapita kasi kama upepo na kusonga mbele:
watu wenye hatia, ambao nguvu zao ndio mungu wao.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.