Habakuki 1:14
Habakkuk 1:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umewafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe wa bahari wasio na mtawala.
Habakkuk 1:14 in English
Habakkuk 1:14 · Berean Standard Bible
You have made men like the fish of the sea, like creeping things that have no ruler.
Context
12Ee Bwana, je, wewe sio wa tangu milele?
Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa.
Ee Bwana, umewachagua wao ili watekeleze hukumu;
Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu. 13Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu,
wala huwezi kuvumilia makosa.
Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu?
Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu
wanawameza wale wenye haki
kuliko wao wenyewe? 14Umewafanya watu kama samaki baharini,
kama viumbe wa bahari wasio na mtawala. 15Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana,
anawakamata katika wavu wake,
anawakusanya katika juya lake;
kwa hiyo anashangilia na anafurahi. 16Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake,
na kuchoma uvumba kwa juya lake,
kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe,
na anafurahia chakula kizuri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.