Native Bible

Habakkuk 1:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake, na kuchoma uvumba kwa juya lake, kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, na anafurahia chakula kizuri.

Habakkuk 1:16 in English

Habakkuk 1:16 · Berean Standard Bible

Therefore he sacrifices to his dragnet and burns incense to his fishing net, for by these things his portion is sumptuous and his food is rich.

Context

14Umewafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe wa bahari wasio na mtawala. 15Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana, anawakamata katika wavu wake, anawakusanya katika juya lake; kwa hiyo anashangilia na anafurahi. 16Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake, na kuchoma uvumba kwa juya lake, kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, na anafurahia chakula kizuri. 17Je, aendelee kuwatoa walio katika wavu wake, akiangamiza mataifa bila huruma?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.