Mwanzo 9:20
Genesis 9:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.
Genesis 9:20 in English
Genesis 9:20 · Berean Standard Bible
Now Noah, a man of the soil, proceeded * to plant a vineyard.
Context
18Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) 19Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia. 20Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 21Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.