Mwanzo 9:22
Genesis 9:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
Genesis 9:22 in English
Genesis 9:22 · Berean Standard Bible
And Ham, the father of Canaan, saw his father’s nakedness and told his two brothers outside.
Context
20Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 21Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 22Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 23Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao. 24Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.