Mwanzo 9:18
Genesis 9:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)
Genesis 9:18 in English
Genesis 9:18 · Berean Standard Bible
The sons of Noah who came out of the ark were Shem, Ham, and Japheth. And Ham was the father of Canaan.
Context
16Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.” 17Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.” 18Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) 19Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia. 20Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.