Mwanzo 37:31
Genesis 37:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu.
Genesis 37:31 in English
Genesis 37:31 · Berean Standard Bible
Then they took Joseph’s robe, slaughtered a young goat, and dipped the robe in its blood.
Context
29Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. 30Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?” 31Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. 32Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.” 33Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.