Native Bible

Genesis 37:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?”

Genesis 37:30 in English

Genesis 37:30 · Berean Standard Bible

returned to his brothers, and said, “The boy is gone! What am I going to do?”

Context

28Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini* za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri. 29Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. 30Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?” 31Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. 32Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.