Mwanzo 37:28
Genesis 37:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini* za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.
Genesis 37:28 in English
Genesis 37:28 · Berean Standard Bible
So when the Midianite traders passed by, his brothers pulled Joseph out of the pit and sold him for twenty shekels of silver * to the Ishmaelites, who took him to Egypt.
Context
26Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini ikiwa tutamuua ndugu yetu na kuificha damu yake? 27Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, nyama yetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali. 28Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini* za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri. 29Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. 30Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.