Native Bible

Genesis 30:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.*

Genesis 30:18 in English

Genesis 30:18 · Berean Standard Bible

Then Leah said, “God has rewarded me for giving my maidservant to my husband.” So she named him Issachar.*

Context

16Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule. 17Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano. 18Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.* 19Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita. 20Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.