Native Bible

Genesis 30:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano.

Genesis 30:17 in English

Genesis 30:17 · Berean Standard Bible

And God listened to Leah, and she conceived and bore a fifth son to Jacob.

Context

15Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kumtwaa mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?” Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.” 16Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule. 17Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano. 18Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.* 19Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.