Mwanzo 3:20
Genesis 3:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.
Genesis 3:20 in English
Genesis 3:20 · Berean Standard Bible
And Adam named his wife Eve,* because she would be the mother of all the living.
Context
18Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,
nawe utakula mimea ya shambani. 19Kwa jasho la uso wako
utakula chakula chako
hadi utakaporudi ardhini,
kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,
kwa kuwa wewe u mavumbi
na mavumbini wewe utarudi.” 20Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai. 21Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 22Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.