Mwanzo 3:18
Genesis 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako, nawe utakula mimea ya shambani.
Genesis 3:18 in English
Genesis 3:18 · Berean Standard Bible
Both thorns and thistles it will yield for you, and you will eat the plants of the field.
Context
16Kwa mwanamke akasema,
“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;
kwa utungu utazaa watoto.
Tamaa yako itakuwa kwa mumeo
naye atakutawala.” 17Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’
“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,
kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo
siku zote za maisha yako. 18Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,
nawe utakula mimea ya shambani. 19Kwa jasho la uso wako
utakula chakula chako
hadi utakaporudi ardhini,
kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,
kwa kuwa wewe u mavumbi
na mavumbini wewe utarudi.” 20Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.