Native Bible

Genesis 27:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.

Genesis 27:15 in English

Genesis 27:15 · Berean Standard Bible

And Rebekah took the finest clothes in the house that belonged to her older son Esau, and she put them on her younger son Jacob.

Context

13Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia, nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.” 14Kwa hiyo alikwenda akawaleta, akampa mama yake, akaandaa chakula kitamu, kama vile alivyopenda baba yake. 15Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. 16Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi. 17Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.