Native Bible

Genesis 27:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka.

Genesis 27:17 in English

Genesis 27:17 · Berean Standard Bible

Then she handed her son Jacob the tasty food and bread she had made.

Context

15Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. 16Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi. 17Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka. 18Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.” Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?” 19Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.