Native Bible

Genesis 26:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi.

Genesis 26:19 in English

Genesis 26:19 · Berean Standard Bible

Then Isaac’s servants dug in the valley and found a well of fresh water * there.

Context

17Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. 18Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa. 19Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,* kwa sababu waligombana naye. 21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.