Mwanzo 26:20
Genesis 26:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,* kwa sababu waligombana naye.
Genesis 26:20 in English
Genesis 26:20 · Berean Standard Bible
But the herdsmen of Gerar quarreled with Isaac’s herdsmen and said, “The water is ours!” So he named the well Esek,* because they contended with him.
Context
18Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa. 19Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,* kwa sababu waligombana naye. 21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.* 22Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,* akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.