Native Bible

Genesis 26:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,* akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”

Genesis 26:22 in English

Genesis 26:22 · Berean Standard Bible

He moved on from there and dug another well, and they did not quarrel over it. He named it Rehoboth * and said, “At last the LORD has made room for us, and we will be fruitful in the land.”

Context

20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,* kwa sababu waligombana naye. 21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.* 22Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,* akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.” 23Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. 24Usiku ule Bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.