Native Bible

Genesis 26:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kutoka pale akaenda Beer-Sheba.

Genesis 26:23 in English

Genesis 26:23 · Berean Standard Bible

From there Isaac went up to Beersheba,

Context

21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.* 22Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,* akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.” 23Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. 24Usiku ule Bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.” 25Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.