Mwanzo 21:4
Genesis 21:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru.
Genesis 21:4 in English
Genesis 21:4 · Berean Standard Bible
When his son Isaac was eight days old, Abraham circumcised him, as God had commanded him.
Context
2Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 4Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 5Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa. 6Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.