Native Bible

Genesis 16:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”

Genesis 16:13 in English

Genesis 16:13 · Berean Standard Bible

So Hagar gave this name to the LORD who had spoken to her: “You are the God who sees me,*” for she said, “Here I have seen the One who sees me!”

Context

11Pia malaika wa Bwana akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli,* kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako. 12Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu, mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu na mkono wa kila mtu dhidi yake, naye ataishi kwa uhasama na ndugu zake wote.” 13Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.” 14Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,* ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi. 15Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.