Mwanzo 16:11
Genesis 16:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia malaika wa Bwana akamwambia: “Wewe sasa una mimba nawe utamzaa mwana. Utamwita jina lake Ishmaeli,* kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.
Genesis 16:11 in English
Genesis 16:11 · Berean Standard Bible
The angel of the LORD proceeded: “Behold, you have conceived and will bear a son. And you shall name him Ishmael,* for the LORD has heard your cry of affliction.
Context
9Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” 10Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.” 11Pia malaika wa Bwana akamwambia:
“Wewe sasa una mimba
nawe utamzaa mwana.
Utamwita jina lake Ishmaeli,*
kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako. 12Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu,
mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu
na mkono wa kila mtu dhidi yake,
naye ataishi kwa uhasama
na ndugu zake wote.” 13Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.