Mwanzo 16:9
Genesis 16:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.”
Genesis 16:9 in English
Genesis 16:9 · Berean Standard Bible
So the angel of the LORD told her, “Return to your mistress and submit to her authority.”
Context
7Malaika wa Bwana akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri. 8Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?”
Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.” 9Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” 10Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.” 11Pia malaika wa Bwana akamwambia:
“Wewe sasa una mimba
nawe utamzaa mwana.
Utamwita jina lake Ishmaeli,*
kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.