Native Bible

Genesis 13:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika.

Genesis 13:16 in English

Genesis 13:16 · Berean Standard Bible

I will make your offspring like the dust of the earth, so that if one could count the dust of the earth, then your offspring could be counted.

Context

14Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. 15Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 16Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. 17Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” 18Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea Bwana madhabahu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.