Mwanzo 11:4
Genesis 11:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”
Genesis 11:4 in English
Genesis 11:4 · Berean Standard Bible
“Come,” they said, “let us build for ourselves a city with a tower that reaches to the heavens, that we may make a name for ourselves and not be scattered over the face of all the earth.”
Context
2Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari* nao wakaishi huko. 3Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 4Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” 5Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. 6Bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.