Mwanzo 11:3
Genesis 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.
Genesis 11:3 in English
Genesis 11:3 · Berean Standard Bible
And they said to one another, “Come, let us make bricks and bake them thoroughly.” So they used brick instead of stone, and tar instead of mortar.
Context
1Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 2Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari* nao wakaishi huko. 3Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 4Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.” 5Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.