Native Bible

Genesis 11:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari* nao wakaishi huko.

Genesis 11:2 in English

Genesis 11:2 · Berean Standard Bible

And as people journeyed eastward,* they found a plain in the land of Shinar * and settled there.

Context

1Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 2Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari* nao wakaishi huko. 3Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 4Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.